Tanzania na Saudi Arabia zasaini mikataba ya ajira kwa Watanzania

0
79

Tanzania imesaini mikataba miwili na Serikali ya Saudi Arabia kwa ajili ya kuajiri Watanzania nchini humo.

Mikataba hiyo imeingiwa wakati wa ziara ya Rais Samia Suluhu nchini Saudi Arabia hivi karibuni ambayo inalenga kuweka mfumo wa kudhibiti mchakato wa kuajiri wafanyakazi wa kitaalam na majumbani, mifumo ya kisheria, mifumo ya kulinda maslahi na haki za wafanyakazi na waajiri, na mifumo rasmi ya kupokea maombi ya ajira.

Vile vile, kamati ya pamoja ya wataalam wa Serikali za Tanzania na Saudi Arabia itaundwa ili kufuatilia utekelezaji wa mikataba ya ajira, kushughulika vikwazo na matatizo yatakayojitokeza, na kuunganisha juhudi za kusuluhisha panapotokea migogoro kati ya waajiri na waajiriwa.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba imesema utaratibu wa kuomba ajira hizo kwa mfumo mpya utatolewa wiki kadhaa zijazo.

Send this to a friend