Tanzania na Uganda kuandaa AFCON 2027

0
41

Tanzania inakwenda kushirikiana na nchi ya Uganda kuomba kuandaa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ya mwaka 2027.

Akizungumza na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Katibu Mkuu wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amesema Tanzania imekubali kushirikiana na Uganda kuomba kuandaa michuano hiyo baada ya kupata ushauri kutoka kwa wakuu wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Timu za Sudan Kusini zakosa viwanja vya nyumbani

Katika mpango huo Tanzania itakuwa na viwanja vinne na Uganda itakuwa na viwanja viwili.

Dkt. Abbasi ameongeza kuwa, Tanzania iko tayari kutuma maombi, pindi CAF itakapofungua milango.

Send this to a friend