Tanzania Prisons na Singida Big Stars zafungiwa kusajili

0
39

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imezifungia kusajili klabu za Ligi Kuu ya NBC za Tanzania Prisons na Singida Big Stars kwa kosa la kusajili wachezaji wenye mikataba na klabu zingine.

Kwa mujibu wa taarifa ya iliyotolewa na Shirikisho leo Oktoba 07, 2022 imesema Klabu ya Tanzania Prisons ilimsajili kipa Musa Mbise wa Coastal Union huku akiwa bado na mkataba na Klabu hiyo.

Kwa upande wa Klabu ya Singida Big Stars kamati imesema ilimsajili kipa Metacha Mnata ambaye pia bado alikuwa ana mkataba na Klabu ya Polisi Tanzania.

Aidha, Kamati imezikumbusha klabu zote nchini kuwa usajili wa wachezaji unafanywa kwa kuzingatia kanuni, na kwa klabu ambazo zitakiuka kanuni hizo zitachukuliwa hatua.

Send this to a friend