Tanzania: The Royal Tour kufikia 86% ya Wamarekani

0
45

Makala ya Tanzania: The Royal Tour iliyozinduliwa jijini New York nchini Marekani inatarajiwa kuwafikiwa asilimia 86 ya Wanarekani, ambao wataona fursa za utalii na uwekezaji nchini Tanzania.

Uzinduzi huo wa aina yake umehudhuriwa na takribani watu 400 na kuhudhuriwa na wakuu wa taasisi za biashara za kimataifa, waongoza utalii wa kimataifa, viongozi wa kisiasa, mashirika ya kimataifa, waandishi wa habari na Watanzania waishio Marekani na wadau wengine.

Shughuli hiyo imeoneshwa mbashara kupitia televisheni za Marekani kwenye mfumo wa utangazaji wa umma (PBS) kupitia kituo cha televisheni cha WTTS chenye watazamaji takribani milioni 3.5 na baadaye makala hayo itaoneshwa kwenye zaidi ya chaneli 300 zinazowafikia takribani asilimia 86 ya Wamarekani.

Makala hiyo itazinduliwa pia jijini Los Angeles Aprili 21, mwaka huu na baada ya matukio hayo mawili, filamu hiyo pia itarushwa kwenye mtandao wa kidijitali wa Amazon na Apple TV.

Kwa Tanzania, makala hiyo itazinduliwa kwanza jijini Dar es Salaam Aprili 28 na baadaye visiwani Zanzibar Mei 7, 2022.

Send this to a friend