Tanzania ya 10 Afrika kwa wanawake kuthamini zaidi urembo

0
38

Utafiti uliofanywa na Sagaci Research umebaini kwamba wanawake nchini Nigeria wanathamini zaidi mwonekano wao wa nje.

Kwa mujibu wa utafiti huo, asilimia 74 ya wanawake wa Nigeria wenye umri kati ya miaka 18 hadi 25 wanatumia muda na pesa nyingi kuboresha mwonekano wao. Kati ya walioulizwa, asilimia 59 walijibu kwamba wana utaratibu wa kila siku wa kutunza ngozi yao kwa sababu wanaamini ni muhimu kuonekana vizuri hadharani.

Uembo pia hauonekani kuwa kipaumbele kwa wanawake vijana nchini Benin, ambapo ni asilimia 30 tu waliripoti kujihusisha na utaratibu wa kila siku wa kutunza ngozi zao.

Hiizi ni nchi 10 za Afrika ambazo wanawake wanathamini zaidi urembo;

1. Nigeria – 74%
2. Uganda – 68%
3. Ghana – 68%
4. Kenya – 66%
5. Afrika Kusini – 66%
6. Misri – 64%
7. Angola- 59%
8. Zambia – 59%
9. Mozambique – 54%
10. Tanzania -54%

Chanzo: Business Insider

Send this to a friend