Tanzania ya Pili Afrika kwa ongezeko la Watalii

0
77

Tanzania imeshika nafasi ya pili Afrika na ya 10 duniani kwa idadi ya watalii wanaoingia nchini, huku idadi ya watalii wakiongezeka kwa asilimia 19 kufikia mwezi Septemba mwaka huu ikiongozwa na Ethiopia ambayo utalii wake umekua kwa asilimia 26.

Ripoti iliyotolewa Novemba 30 mwaka huu ya Shirika la Umoja wa Mtaifa la Utalii Duniani iitwayo “World Tourism Barometer” imebainisha kuwa idadi hiyo inalinganishwa na idadi ya juu iliyopata kufikiwa ambayo ni kabla ya janga la Uviko-19 mwaka 2019.

Aidha, katika kipengele cha mapato ya sekta ya Utalii, Tanzania imekuwa ya 10 duniani na ya tatu Afrika (ikiwa nyuma ya Mauritius na Morocco kwa Afrika) katika nchi ambazo zimeongeza kwa kiwango kikubwa mapato yake ikilinganishwa na mwaka 2019 ambapo ripoti hiyo inaonesha kwa Tanzania yameongezeka kwa asilimia 26.

Hata hivyo, kidunia Qatar imeongoza kwa idadi ya watalii ikifuatiwa na Saudi Arabia, Andora, Albania huku mataifa mengi makubwa duniani yakionekana bado yanasuasua kurejea katika takwimu za kabla ya Uviko-19.

Send this to a friend