Tanzania yaamriwa kufuta adhabu ya viboko

0
42

Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) imetoa agizo kwa Serikali ya Tanzania kufuta adhabu ya viboko kwa wanaotiwa hatiani kwa makosa mbalimbali, kwani adhabu hiyo inachukuliwa kuwa ni utesaji na udhalilishaji. Serikali imepewa muda wa miezi sita kutekeleza uamuzi huu.

Uamuzi huo umetokana na kesi iliyowasilishwa na raia wa Tanzania, Yassin Maige, ambaye alihukumiwa mwaka 2003 kutumikia kifungo cha miaka 30 na kuchapwa viboko 12 kwa kosa la wizi wa kutumia silaha katika mkoa wa Tabora. Mahakama imetoa agizo la kulipa fidia ya TZS 300,000 kwa Yassin Maige kutokana na kudhalilishwa na adhabu aliyopewa.

Majaji wa AfCHPR wametoa wito kwa Serikali kufuta adhabu ya viboko na kuzingatia Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu, ambao unakataza adhabu za utesaji, ukatili, unyama, na udhalilishaji.

Ufaransa yapiga marufuku iPhone 12

Kwa kuongezea, jopo la majaji hao limeagiza mamlaka husika kuwasilisha ripoti ya utekelezaji wa uamuzi huu kila baada ya miezi sita, hadi pale mahakama itakaporidhika na utekelezaji wa agizo hilo.

Send this to a friend