Tanzania yaijibu Umoja wa Ulaya suala la bomba la mafuta kutoka Uganda

0
44

Serikali imesema hakutakuwa na athari zozote za kimazingira wakati wa utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha Mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima Uganda hadi Chongoleani Tanga kwani tahadhari zote zilizingatiwa kitalaamu.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nishati, Januari Makamba Septemba 16, 2022 ikiwa ni sehemu ya ufafanuzi wa maazimo yaliyotolewa siku tatu na Bunge la Ulaya (EU) kuhusu utekelekezaji wa mradi huo.

EU imetoa maazimio saba ikiwamo madai ya mradi huo kutozingatia viwango vya kimataifa katika kulinda haki za binadamu na mabadiliko ya tabianchi, kutolipa fidia huku ikishinikiza kulinda haki za wanaharakati wa mazingira.

Taarifa ya TACAIDS kuhusu dawa za kuzuia maambukizi ya Ukimwi

Akitoa ufafanuzi, Waziri Makamba amesema hakuna ardhi itakayochukuliwa na mradi bila kufanyiwa fidia zinazokadiriwa kuwa shilingi bilioni 23 kwa wakazi 9,122.

“Utwaaji ardhi unazingatia Sheria zote mbili za Tanzania na viwango vya utendaji vya Shirika la Fedha la Kimataifa. Tanzania wapo watu 9,513 walioathiriwa na mradi na 331 za kuhamishwa kwa chaguo la makazi au fidia ya pesa taslimu. Takriban asilimia 85 yao wamechagua kwa makazi na ujenzi unaendelea,” amesema Waziri Makamba.

Send this to a friend