Tanzania yajidhatiti kuendelea kukuza amani na usalama Afrika

0
46

Rais Samia Suluhu Hassan amesema jitihada za pamoja ni muhimu katika kukabiliana na changamoto za kiusalama zinazokabili Bara la Afrika na katika kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi ndani ya bara Afrika.

Ameyasema hayo kwenye mkutano wa kuadhimisha miaka 20 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU) katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam ambapo Rais Samia ndio mwenyekiti wa baraza hilo kwa mwezi Mei, 2024.

Akitoa hotuba yake, Rais Samia amesema tangu kuanzishwa kwa Baraza hilo mwaka 2004, limepata mafanikio mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuanzisha majadiliano ya upatanishi na kusaidia nchi kujengwa upya baada ya vita, kukabiliana na migogoro na matishio mbalimbali pamoja na kuchangia juhudi za bara la Afrika katika kukabiliana na ugaidi.

“Katika ngazi za kitaifa, baraza limeshirikiana na nchi zinazokabiliwa na changamoto za amani na usalama na kufanya ziara katika nchi hizo na ziara hizo zimeliwezesha baraza kuelewa vyema changamoto za kiusalama, kusikiliza kutoka kwa wanaohusika na migogoro hiyo na kuonesha mshikamano kwa waathirika wa migogoro hiyo,” ameeleza.

Aidha, Rais Samia amesema Tanzania itaendelea kukuza amani na usalama barani Afrika ili kuweka mazingira stahiki ya kujenga ustawi wa kijamii na kiuchumi wa watu wetu.

Send this to a friend