Tanzania yakaribisha wawekezaji sekta ya nishati

0
49

Tanzania imekaribisha wawekezaji kutoka kote duniani kuja kuwekeza kwenye sekta ya nishati kutokana na uwepo fursa nyingi kuanzia kwenye uzalishaji hadi usambazaji wa nishati maeneo mbalimbali nchini.

Mwaliko huo umetolewa na Waziri wa Nishati, January Makamba jijini Dar es Salaam katika mkutano wa wadau wa sekta ya nishati, wawekezaji, kampuni za nishati kutoka nje ya nchi, mabalozi wa nchi mbalimbali ambao unaoangazia hali ya sekta ya nishati sambamba na maendeleo yaliyofikiwa.

Akieleza kwanini wawekezaji waichague Tanzania, na kwanini sasa ni muda sahihi zaidi, Makamba amesema “Tanzania ni mahali sahihi penye amani katika kufanya uwekezaji, hivyo tunawakaribisha wawekezaji wenye tija kuwekeza kwenye sekta ya nishati nchini.”

Wadau mbalimbali walioshiriki mkutano huo wamepongeza namna Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha sekta hiyo yenye mchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii pamoja na kutatua changamoto zinazoikabili ikiwemo urasimu.

Mkutano huo umeandaliwa na EnegeryNet  ikishirikiana na Wizara ya Nishati, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Baadhi ya picha mbalimbali kutoka katika ufunguzi wa mkutano huo;

Send this to a friend