Tanzania yalamba dume Umoja wa Afrika

0
31

Mkutano wa 35 wa Wakuu wa Nchi na Serikali umeridhia na kupitisha ombi la Tanzania la kutaka Kiswahili kuwa lugha ya kazi katika umoja huo.

Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango aliwasilisha ombi hilo akieleza kuwa Kiswahili ni miongoni mwa lugha  za kiafrika zenye wazungumzaji wengi barani Afrika ambapo takribani watu milioni 100 wanakitumia pamoja na wazungumzaji kutoka nje ya Bara la Afrika.

Mkutano huo pia umeichagua Tanzania kuwa mjumbe wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU)

Pamoja na mambo mengine mkutano huo wa 35 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja Afrika (AU) nchi wanchama zimelaani vitendo vya uvunjaji katiba uliopelekea mapinduzi ya kijeshi katika mataifa mbalimbali pamoja na vitendo vya ugaidi vinavyoendelea katika mataifa mbalimbali barani Afrika. Umoja wa Afrika umeasa majadiliano kuendelea katika nchi hizo ili kurejesha utawala wa kiraia na kidemokrasia.

Katika kupambana na UVIKO19, Umoja wa Afrika umetoa rai kwa nchi kushirikiana katika kukabiliana na janga hilo ikiwemo kuhakikisha chanjo zinapatikana pamoja na kuyaunga mkono mataifa yalioanza jitihada za kuzalisha chanjo hiyo barani Afrika ikiwemo Afrika Kusini, Senagal na Rwanda.

Send this to a friend