Tanzania imeomba ridhaa ya kuwa makao makuu ya Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya Nne (AUSC) kwa wajumbe wa mkutano wa wataalamu wa michezo kutoka katika kanda hiyo.
Amesema hayo Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu wakati akifungua kikao cha wataalamu hao Mei 02, mwaka huu jijini Arusha ambapo amesisitiza kuwa Serikali ya Tanzania ina nia na kila sababu ya kuwa makao makuu ya kanda hiyo na endapo itapewa ridhaa hiyo ina uwezo wa kuhudumia sekretarieti hiyo.
TFF yasogeza mbele mechi za nusu fainali ya kombe la shirikisho
“Kutokana na mipango thabiti iliyopo ndani ya Serikali yetu inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluh Hassan ya kuendeleza diplomasia kupitia michezo, tunaomba kuwa makao makuu ya Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika ili kutekeleza azma hiyo ya Serikali,” amesema Yakubu.
Ameongeza kuwa Tanzania ina nia ya dhati ya kuanzisha mashindano ya kanda hiyo pamoja na kuanzisha tuzo maalumu za michezo ndani ya kanda iwapo itachaguliwa, kwa lengo la kusaidia kuinua michezo katika kanda hiyo.