Tanzania yapongezwa namna Bandari ya Dar inavyohudumia Afrika Mashariki

0
42

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat amesema anategemea kuwa kama Tanzania ilivyokuwa kinara kwenye ukombozi wa Afrika basi itakuwa kinara pia katika kuchangamkia fursa ya Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) katika kukuza biashara ikizingatiwa kuwa kupitia miundombinu yake ya bandari imeweza kurahisisha biashara kwa nchi jirani zinazotumia bandari hiyo.

Amesema Tanzania ni kitovu muhimu cha kuunganisha nchi jirani kibiashara na usafirishaji wa bidhaa mbalimbali katika nchi hizo kutokana na jiografia yake.

Katika hatua nyingine, amempongeza Rais Samia kwa uongozi wake tangu aingie madarakani na jitihada zake za kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo.

Kwa upande wake, Rais Samia Suluhu Hassan amemueleza Faki kuwa Tanzania haikuachwa nyuma na athari za UVIKO 19 kiuchumi, lakini inajitahidi kukabiliana na athari hizo kupitia njia mbalimbali ili kuhakikisha uchumi wake unaimarika.

Rais Samia amesema ni wakati sasa kwa nchi za Afrika kutumia fursa zilizopo baada ya athari za UVIKO 19 kujiimarisha kiuchumi kwasababu nchi hizo zina fursa nyingi kiuchumi.

Send this to a friend