Tanzania yashika nafasi ya 10 Afrika kwa mamilionea wengi wa dola

0
49

Tanzania imeshuka katika idadi ya mamilionea wa dola hadi nafasi ya 10 kutoka nafasi ya saba mwaka 2022, kulingana na ripoti ya kampuni ya utafiti ya New World Wealth and Henley & Partners iliyotolewa Machi 29 mwaka huu.

Ikiwa na ukuaji wa asilimia 20 katika kipindi cha miaka 10 [2012–2022], ripoti ya hivi karibuni imeonesha Tanzania ina watu 2,400 wenye thamani ya dola milioni 1 [TZS bilioni 2.3] na zaidi, watu 6 wenye thamani ya zaidi ya dola milioni 100 [zaidi ya TZS bilioni 230], na mtu mmoja mwenye thamani ya zaidi ya dola bilioni moja (zaidi ya TZS trilioni 1.3].

TRC yasitisha huduma ya usafiri wa treni

Tanzania imesalia kuwa nchi pekee Afrika Mashariki yenye bilionea wa dola huku mamilionea wengi wa dola (1,300) wakiishi katika mji mkuu wa kibiashara, Dar es Salaam, jiji lililoorodheshwa katika nafasi ya 12 kwa utajiri mwaka 2022, likiwa na jumla ya utajiri binafsi wa wananchi wa dola bilioni 24 [TZS trilioni 55].

Licha ya kudorora kwa mamilionea wa dola za Tanzania ikilinganishwa na mwaka jana, Tanzania ina ongezeko la asilimia 20 katika idadi ya mamilionea wa dola tangu 2012 licha ya nchi zingine kushuka kwa kasi.

Send this to a friend