Tanzania yashika nafasi ya 5 uvutaji bangi nyingi Afrika

0
80

Ripoti ya hivi karibuni kuhusu matumizi ya tumbaku iliyofanywa na kikundi cha kampeni ya afya ya umma na wasomi wa Marekani imegundua kuwa viwango vya uvutaji sigara vinaongezeka miongoni mwa watu wazima na vijana katika baadhi ya nchi barani Afrika.

Matumizi ya dawa za kulevya ni ya juu miongoni mwa vijana kuliko wazee. Zaidi ya hayo, ripoti ya 2021 ya Umoja wa Mataifa kuhusu matumizi ya madawa ya kulevya pia ilithibitisha kwamba idadi ya watumiaji wa madawa ya kulevya barani Afrika inakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 40 ifikapo mwaka 2030.

Kwa mujibu wa ripoti ya kimataifa ya matumizi ya bangi ya New Frontier Data, hizi ni nchi 10 za Afrika zinazoongoza kuwa na watumiaji wengi wa bangi;

1. Nigeria – Milioni 20.8

2. Ethiopia – Milioni 7.1

3. Misri – Milioni 5.9

4. DR Congo – Milioni 5

5. Tanzania – Milioni 3.6

6. Kenya – Milioni 3.3

7. Sudan – Milioni 2.7

8. Uganda – Milioni 2.6

9. Madagascar – Milioni 2.1

10. Ghana – Milioni 2

Nchi za Afrika zenye idadi ndogo ya watumiaji wa bangi ni pamoja na Zimbabwe, Malawi, Niger na Zambia, zenye watumiaji milioni 1.1, milioni 1.2, milioni 1.2 na milioni 1.4, mtawalia.