Tanzania yashika nafasi ya pili unywaji pombe Afrika

0
19

Baadhi ya tamaduni huona unywaji pombe kuwa jambo la kufurahisha, ilhali tamaduni nyingine huona ulevi kuwa ni dhambi.

Mwaka 2019 Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitoa ripoti kamili kuhusu hali ya matumizi ya pombe duniani ili kusaidia nchi kupambana na matumizi mabaya ya pombe na kuepuka madhara mabaya kwa afya na jamii.

Kulingana na ripoti hiyo, watumiaji wakubwa wa pombe ni nchi za Ulaya ya Kati, Pasifiki Kusini, na sehemu za Caribbean. Ripoti ilibainisha kwamba barani Ulaya, bia na divai ni maarufu sana, na nchi nyingi zinazotumia pombe nyingi pia ni wazalishaji wakubwa kama vile Ufaransa na Ujerumani.

Nchi 10 za Afrika zenye bei kubwa zaidi ya mafuta

Lakini kuna nchi kama Bangladesh, Saudi Arabia, Kuwait na nchi nyingine za Kiislamu ambazo ulevi umepigwa marufuku kwa sababu ni kinyume na matakwa ya dini.

Hapa kuna orodha ya nchi 10 za Kiafrika zenye matumizi makubwa ya pombe;

1. Seychelles
2. Tanzania
3. Eswatini
4. Burkina Faso
5. Afrika Kusini
6. Uganda
7. Gabon
8. Rwanda
9. Equatorial Guinea
10. Botswana

Chanzo: Business Insider