Tanzania yasitisha safari za Shirika la Ndege la Kenya

0
41

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imetangaza kusitisha vibali vya Shirika la Ndege la Kenya (KQ) kuendesha safari za abiria kati ya Nairobi na Dar es Salaam kuanzia Januari 22, mwaka huu.

Hii ni kufuatia uamuzi wa mamlaka ya anga ya Kenya kukataa ombi la Tanzania la safari za ndege za mizigo kutoka Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) lililotaka kufanya safari kati ya Nairobi na mataifa mengine, jambo ambalo limetajwa kuwa kinyume na Kifungu cha 4 cha Mkataba wa Maelewano kuhusu Huduma za Ndege kati ya Tanzania na Kenya yaliyotiwa saini Novemba 24, 2016 jijini Nairobi, Kenya.

“Kufuatia uamuzi huu, hakutakuwa na safari za ndege za abiria kwa KQ kati ya Nairobi na Dar es Salaam kuanzia tarehe 22 Januari 2024,” imeeleza taarifa.

Imeongeza kuwa “Jamhuri ya Muungano wa Tanzania daima itajitahidi kuzingatia kanuni za Mkataba wa Chicago 1944 na Makubaliano ya Huduma za Anga baina ya nchi mbili.”

Send this to a friend