Tanzania yatajwa kuwa nchi yenye mafanikio ya demokrasia na utawala bora

0
61

Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa nchi barani Afrika ambazo zimepata mafanikio makubwa katika kuimarisha demokrasia na dhana ya utawala bora katika kuwatumikia wananchi wake.

Ameyasema hayo Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Juma Ali Khatib wakati alipokutana na uongozi wa taasisi ya mpango wa hiari wa nchi za umoja wa Afrika kujipima katika vigezo vya utawala bora (APRM) Tanzania katika ofisi ya baraza la wawakilishi Mjini Unguja.

Khatib amesema taswira ya Tanzania katika masuala ya demokrasia na utawala bora inatokana na msimamo mahiri wa Rais Samia Suluhu kwa kuonesha ukomavu wa hali ya juu katika suala la demokrasia na kuruhusu ushirikishwaji wa wananchi.

Utafiti: Asilimia 63 ya Watanzania wanafurahia Serikali inavyosimamia uchumi

“Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepiga hatua kubwa katika kukuza na kuimarisha utawala bora na demokrasia, hatua ambayo imeruhusu tena kuwepo kwa mikutano ya hadhara ya kiasiasa ambayo huviwezesha vyama kuwasiliana na wanachama wao kuhusu sera na malengo yao,” amesema.

Aidha, ametoa rai kwa vyama vya siasa kutumia nafasi ya mikutano ya hadhara kunadi sera zao kwa wananchi na kuelezea malengo ya vyama vyao na si kunadi matusi.