Tanzania yatoa tahadhari kwa Watanzania waliopo Mashariki ya Kati

0
7

Serikali imetoa tahadhari kwa Watanzania wanaoishi au kusafiri katika eneo la Mashariki ya Kati, ikiwemo Bahrain, Israel, Kuwait, Qatar, Falme za Kiarabu (UAE) na Oman, ikiwataka kuepuka safari za kwenda au kutoka katika kipindi hiki cha taharuki ya kiusalama.

Katika taarifa hiyo, Serikali imewasisitiza Watanzania walioko katika ukanda huo kubaki katika makazi yao kwa sasa, kuepuka maeneo yenye shughuli za kijeshi pamoja na kufuata kwa makini maelekezo yanayotolewa na mamlaka husika katika nchi wanazoishi.

Pia, imewataka kutumia njia rasmi za mawasiliano na taarifa pamoja na kuhifadhi pasipoti zao na vitambulisho sehemu salama na inayopatikana haraka endapo kutatokea dharura.

Aidha, imeeleza kuwa katika nyakati kama hizi za changamoto za kiusalama, utoaji wa huduma za kibalozi ana kwa ana unaweza kuwa na mipaka kulingana na hali halisi ya usalama katika maeneo husika.