Tanzania yaueleza Umoja wa Mataifa ilivyoboresha sekta ya elimu

0
24

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amesema katika kuelekea mwaka 2030, mataifa yanapaswa kujitoa upya na kuazimia kuongeza uwekezaji zaidi katika sekta ya elimu kwa nia ya kuhakikisha watoto wanapata elimu iliyo bora na ya uhakika.

Amesema hayo wakati akitoa hotuba katika Mkutano wa Baraza Kuu la 77 la Umoja wa Mataifa (UNGA) uliobeba ajenda ya Mageuzi katika sekta ya elimu ulioshirikisha wakuu wa nchi na serikali kutoka mataifa mbalimbali, wakuu wa taasisi na mashirika pamoja na wadau wa elimu.

Makamu wa Rais amesema kupatikana kwa elimu bora kutapunguza matabaka katika ajira pamoja na kipato baina ya wananchi.

Serikali kuandaa ramani mpya ya Tanzania

Amesema tayari Tanzania imechukua hatua mbalimbali katika kuboresha sekta ya elimu ikiwemo kuanza mchakato wa kuboresha mitaala kwa kuwashirikisha wadau wa elimu, kuwekeza katika vyuo vya ufundi stadi na mafunzo, kutoa elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari pamoja na kuongeza bajeti ya wizara husika kufikia asilimia 18 ya bajeti yote ya serikali.

Ameongeza kwamba kwa kuzingatia maendeleo ya sayansi na teknolojia, Serikali pia imedhamiria kuboresha usimamizi wa nguvu kazi ya walimu ili kuboresha ufundishaji na ujifunzaji bora kwa kuwajengea uwezo walimu na maofisa elimu kuhusu uunganishaji wa teknolojia katika ufundishaji na ujifunzaji pamoja na uandaaji wa masomo ya kidijitali.

Send this to a friend