Tanzania yazuia kampuni 3 za ndege za Kenya kuingia nchini

0
38

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imezuia makampuni matatu ya ndege ya Kenya kufanya safari zake nchini, kutokana na mzozo baina ya matafai hayo makubwa ya Afrika Mashariki.

Akitolea ufafanuzi wakati akizungumza na gazeti la The Citizen, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari amesema kampuni zilizozuiwa ni AirKenya Express, Fly540 na Safarilink Aviation zote kutoka Nairobi.

“Sababu za maamuzi ya kuondoa ruhusa kwa kampuni tatu za ndege za Kenya ni mgogoro unaoendelea kati ya nchi hizi,” amesema Johari.

Hivi karibuni Kenya ilitoa orodha ya nchi 130 ambazo raia au wageni wake hawatotakiwa kukaa karantini kwa siku 14, huku Tanzania ikikosekana kwenye orodha hiyo.

August 1, 2020, TCAA iliipiga marufuku Shirika la Ndege la Kenya, Kenya Airways (KQ) kufanya safari zake nchini Tanzania, maamuzi ambayo TCAA ilisema ni kujibu Kenya kwa Tanzania kuondolewa kutoka kwenye nchi zenye ruhusa ya wageni wake kupokelewa Kenya bila kupitia vizuizi vya Covid19.

Send this to a friend