Updated: Askofu Getrude Rwakatare afariki dunia

0
40

Askofu Dkt. Getrude Rwakatare wa Kanisa la Mlima wa Moto amefariki dunia leo alfajiri Aprili 20, 2020 katika Hospitali ya Rabininsia jijini Dar es Salaam.

Pamoja na nyadhifa mbalimbali alizokuwa nazo kabla ya kukutwa na umauti, pia alikuwa alikuwa Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Dkt. Rwakatare alizaliwa Disemba 31, 1950.

Kwa mujibu wa watoto wake, mama yao alikuwa akisumbuliwa na presha pamoja na tatizo la moyo.

Muta Rwakatare ambaye ni mtoto wa marehemu amesema kuwa hadi jana usiku hali ya mama yake haikuwa mbaya, na aliweza na kwenda kulala akiwa vizuri, lakini usiku zaidi hali yake ilibadilika ikawa mbaya zaidi.

Aidha, ameongeza kuwa kwa sasa wanasubiria vipimo vya hospitali, kisha watakaa kikao cha familia kujua nini kinaendelea.

Taarifa zaidi zitakujia, endelea kuwa nasi.

Send this to a friend