Tanzia: Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani afariki dunia

0
55

Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania Augustino Ramadhani amefariki dunia leo Aprili 28, 2020 katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Jaji Ramadhani aliteuliwa na Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo mwaka 2006 na alistaafu mwaka 2010.

Mbali na wadhifa huo, amewahi kutumikia nyadhifa mbalimbali kama vile Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania Bara, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar.

Alizaliwa visiwani Zanzibar, Mtaa wa Kisima Majongoo kwenye familia ya watoto wanne wa Mwalimu Mathew Douglas Ramadhani na Bridget Anna Constance Masoud akiwa ni mtoto wa pili katika familia hiyo.

Send this to a friend