Tanzia: Mzee Njenje wa Bendi ya Kilimanjaro afariki dunia

0
48

Mwanamuziki mkongwe aliyekuwa mmoja wa wanaounda Bendi ya Kilimanjaro (Wana Njenje), Mabrouk Omar, maarufu Mzee Njenje amefariki dunia.

Mzee Njenje ambaye ametamba na vibao vingi ikiwa ni pamoja na Njenje, Kinyaunyau wamefariki leo Mei 24, 2020 alfajiri jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Marehemu alikuwa akisumbuliwa na Ugonjwa wa Kiharusi kwa takribani miaka mitano.

Mazishi yake yanatarajiwa kufanyika katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo saa 10 jioni.

Send this to a friend