Tanzia: Rais wa Burundi afariki dunia

0
45

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza (55) amefariki dunia. Taarifa ya serikali imeeleza kuwa alikuwa hospitali akisumbuliwa na tatizo la moyo.

Kiongozi huyo amefariki ikiwa ni siku chache kabla ya kung’atuka madarakani kutokana na nchi hiyo kufanya uchaguzi karibuni na kuchagua Rais mpya.

Taarifa ya Msemaji wa Serikali ya Burundi, Balozi Willy Nyamitwe imesema  Rais Nkurunzima amefariki kwa mshtuko wa moyo tofauti na taarifa zilizokuwa zinazagaa kwenye vyombo vya habari.

Serikali ya Burundi imetangaza siku saba za maombolezo  na kuwataka wananchi wa taifa hilo kuwa katika utulivu wakati mipango mingine ikifanyika.

Send this to a friend