Tarime: Auawa kwa kisu akigombania mwanamke baa

0
50

Mkazi wa Kijiji cha Sirari, wilaya ya Tarime mkoani Mara, John Nyamesati ameuawa kwa kuchomwa kisu wakati akigombea mwanamke baa kisha mtuhumiwa kutokomea kusikojulikana.

Akizungumza kaka wa marehemu, Yohana Nyamesati amesema mdogo wake alichomwa kisu Juni 22 mwaka huu katika baa ya Chacha Gitwi ambapo kulitokea ugomvi wa kugombea mwanamke na mtuhumiwa Charles Gatangenyi ambaye baada ya kutenda tukio hilo alitokomea kusikojulikana.

“Askari walifika na gari na kumchukua John akiwa anatokwa na damu, alipofika hospitali ya Wilaya alikuwa amekwishafariki dunia. Marehemu ameacha wake watatu na watoto wanne. Ametuachia mzigo wa kuwatunza,” ameeleza.

Amwagiwa tindikali akidai kugawana mali na mumewe

Diwani wa Kata Kenyamanyori, Farida Nchagwa ametoa wito kwa vijana kuacha tabia ya kubeba silaha wanapokuwa katika maeneo yenye vilevi ili kuepusha madhara ikiwemo kifo.

Naye Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Tarime, ACP. Michael Njera amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kueleza kuwa polisi wanaendelea na upelelezi ili kumtia mbaroni mhusika.