Tatizo la moyo kutanuka na sababu zake

0
101

Moyo kutanuka kitaalamu ‘cardiomegally’ maana yake moyo wako umekuwa mkubwa kupita kiwango cha kawaida. Moyo unatanuka pale misuli yake inapofanya kazi kupita kiasi mpaka kupanuka na kufanya chemba za moyo nazo kupanuka.

Moyo uliotanuka hauwezi kusambaza damu vizuri kwenye maeneo mbalimbali ya mwili ukilinganisha na moyo mzima. Kitendo hichi kinakuweka kwenye hatari ya kupata kiharusi na hata moyo kufeli.

Hali zinazoweza kusababisha kupanuka kwa moyo ni pamoja na:

Tatizo la moyo ulilozaliwa nalo au kuharibika kwa moyo kutokana na mshtuko wa moyo, kudhoofu kwa misuli ya moyo au moyo kutodunda kwa mpangilio huweza kusababisha moyo kutanuka.

Kupanda kwa shinikizo la damu
Hali hii husababisha moyo kusukuma damu kwa nguvu zaidi ili kuifikisha sehemu mbalimbali za mwili. Kupanda kwa shinikizo la damu kunaweza kusababisha ventrikali ya kushoto kupanuka na kufanya misuli ya moyo kudhoofika.

Wakati mzuri wa kunywa maji kwa siku

Ugonjwa wa misuli ya moyo
Ugonjwa huu husababisha misuli ya moyo kukakamaa na kusababisha moyo kujaribu kusukuma damu kwa nguvu zaidi na kusababisha moyo kutanuka.

Kupanda kwa shinikizo la damu kwenye mshipa wa damu unaounganisha moyo na mapafu.  Hali hii hujulikana kitaalamu kama Pulmonary Hypertension. Hii husababisha moyo kusukuma damu kwa tabu kwenda na kutoka kwenye mapafu ambako huwekewa hewa ya oksijeni.

Sababu nyingine ni;
•Maambukizi ya virusi kwenye moyo
•Ukuaji wa valve za moyo usio wa kawaida
•Mimba, hasa wakati wa kujifungua
•Magonjwa ya figo
•Matumizi makubwa ya pombe na dawa za kulevya
•Maambukizi ya virusi vya Ukimwi
•Matatizo ya kurithi
•Matatizo ya tezi ya shingoni (thyroid)
•Upungufu wa damu

Baadhi ya watu wenye moyo mkubwa hawana dalili za moja kwa moja, ingawa wengi hupata dalili kama kupumua kwa tabu, mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida, kujaa au kuvimba kwa mwili hasa miguu, wakati mwingine vidole kufa ganzi na kukakamaa.

Dalili nyingine ni kifua kubana au kuuma, kupata kizunguzungu, kuhisi hali ya mwili kunyong’onyea au kutokuwa na nguvu, kupoteza fahamu na kuzimia.

Send this to a friend