Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), limetangaza kuanza kutoa tuzo kwa wasanii wakongwe na kizazi kipya kwa lengo la kutambua mchango wao katika jamii kupitia sanaa yao.
Ameyasema hayo leo Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba katika kipindi cha Jambo Tanzania, wakati akifananua kuhusu tamasha la Tukutane Kwetu litakalofanyika Mei 21 mwaka huu.
“Sisi TBC ndio baba wa sanaa, tumeanza kupiga nyimbo za wasanii miaka ya nyuma kabisa, hivyo lazima tuwapongeze kwa kazi wanazofanya na hii si kwa wakongwe tu hata hawa wapya, lengo ni kutambua mchango wao katika sanaa,” amesema Dkt. Rioba
Tanzania yanyemelea fursa ya kuandaa Tuzo za MTV 2023
Aidha, shirika hilo limebainisha kwamba linafanya hivyo ili kuenzi na kuthamini kazi zianazofanywa na wasanii.