TBC sio mali ya serikali wala CCM- Naibu Waziri, Juliana Shonza

0
41

“Shirika la Habari Tanzania (TBC) ni chombo cha umma, hakina itikadi za chama, dini wala kabila. Kuna dhana Watanzania na upinzani wanayo kuwa TBC inamilikiwa na serikali, au CCM, hii si sahihi, kwani inafanyakazi na watu wote.”

Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza alipokuwa akijibu tuhuma zilizoibuliwa na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aliyedai kuwa TBC imekuwa ikibagua vyama vya upinzani.

Shonza amesema kuwa dhani hiyo si sahihi na kusema kuwa chombo hicho kinafanya kazi na watu wote, makundi na taasisi zote, na kuvitaka vyama vya upinzani kupeleka taarifa zao badala ya kulalamika tu.

Akitolea mfano jambo hilo, Shonza amesema hivi karibuni TBC ilirusha Mkutano Mkuu wa NCCR-Mageuzi, chama ambacho ni cha upinzani, jambo linaloonesha kuwa chombo hicho hakina upinzani.

Msikilize hapa chini akitoa ufafanuzi zaidi:

Send this to a friend