TBS: Johnson’s Baby Powder inayodaiwa kusababisha saratani hazipo nchini

0
24

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limesema lilifanya ukaguzi katika maduka mbalimbali nchini na kujiridhisha kuwa toleo namba 22318RB la bidhaa za Johnson’s Baby Powder inayodaiwa kuwa na madini yanayosababisha saratani halikuingia nchini na halipo katika soko.

Taarifa hizo zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zimedai bidhaa hiyo inayozalishwa kwa kutumia kiambato cha talc inadaiwa kuwa na uchafuzi wa madini ya asbestos yanayosababisha saratani.

Kampuni ya Johnson & Johnson inayozalisha bidhaa hizo imetangaza rasmi kusitisha matumizi ya kiambato hicho katika uzalishaji wake duniani kote, na badala yake kutumia kiambato cha comstarch.

Halikadhalika, TBS imesema inachukua hatua ya tahadhari na kuwaelekeza wananchi kutoendelea kutumia bidhaa za Johnson’s Baby Powder zenye kiambato hicho kama ilivyokwishaelezwa awali kupitia vyombo vya Habari.

“Waigizaji, wasambazaji na wauzaji wa bidhaa hizo wanaelekezwa kusitisha uingizaji nchini, uuzaji na usambazaji wa bidhaa za Johnson’s Baby Powder zenye kiambato cha talc,” imeeleza taarifa ya TBS.

Send this to a friend