TBS kukichukulia hatua kiwanda kinachozalisha Safari Premium Tea

0
44

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limesema hatua stahiki zitachukuliwa juu ya kiwanda cha Afri Tea and Coffee Blenders kinachozalisha bidhaa ya Safari Premium Tea baada ya kuingiza malighafi kutoka nchini Kenya bila kutoa taarifa kwa TBS.

Taarifa hiyo imefuatia baada ya taarifa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha utata unaotokana na taarifa iliyoko kwenye kifungashio na uasili wa bidhaa ya majani ya chai aina ya Safari Premium Tea pamoja na matumizi ya alama ya TBS inayoingizwa kutoka Kenya na kufungashwa nchini.

Kenya yabaini uwepo wa Mbu asiyekufa kwa dawa za Afrika

TBS imeeleza kuwa bidhaa hiyo imepewa leseni namba 1595 ya kutumia alama ya ubora ya TBS kwenye bidhaa za Blended Black Tea (Green Label Tea, Kilimanjaro, African Pride, Simba Chai, Simba Chai Tangawizi, Safari Premium Tea) tangu mwaka 2014 na bidhaa zote zinazalishwa Tanzania na kwa kutumia malighafi zilizoko nchini.

Aidha, TBS imesema kufuatia taarifa hiyo ilifanya ukaguzi wa dharura kiwandani Februari 20, 2023 na kujiridhisha kwamba mzalishaji aliingiza chai kama malighafi kutoka Kenya mwezi Oktoba 2022, bila kutoa taarifa kwa TBS kama mkataba unavyotaka.

Send this to a friend