TBS: Matairi ya magari mengi yanayoingizwa nchini yameisha muda

0
39

Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Lazaro Msasalaga amesema kuwa magari mengi yanayoagizwa nchini yana matairi ambayo yamekwisha muda wake wa matumizi.

Akizungumza katika mkutano wa viongozi wa shirika hilo na wahariri wa vyombo vya habari, amesema matairi huandikwa tarehe ya kuisha muda wake na kwamba magari mengi yanayoagizwa nchini yana matairi ambayo yamekwisha muda, huku baadhi ya wamiliki wakishindwa kuyabadili hali ambayo ni hatari.

“Hata kama hayajatumika, iwapo muda wake umeisha haifai kutumika tena, lakini bahati mbaya baadhi ya watu wanapenda njia za mkato ili kuendelea kutumia matairi yaliyoisha muda wake” amesema Lazaro.

Lazaro amelaani tabia za baadhi ya wamiliki wa magari ambao  hushindwa kurudi bandarini kutoa taarifa baada ya kutakiwa kufanya marekebisho na badala yake hutafuta njia nyingine ili kuendelea kutumia matairi hayo.

Send this to a friend