TBS yawataka wauzaji wa chakula na vipodozi kujisajili

0
43

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limewataka wafanyabiashara wote wanaojihusisha na biashara za chakula na vipodozi kujisajili na kupewa vibali vya usajili wa jengo (premise registration permits).

TBS imesema kuwa maeneo yanayopaswa kuombewa vibali hivyo ni pamoja na hoteli za kawaida na za kitalii, maduka makubwa, maduka ya jumla na rejareja ya chakula na vipodozi.

Maeneo mengine ni mashine ndogo za kusaga nafaka zisizofungasha (posh mills) vibanda, watoa huduma za chakula kwenye mikusanyiko, baa na magari ya kubebea vyakula na vipodozi.

Maombi yote yanatakiwa kuwasilishwa kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya TBS (www.tbs.go.tz) au mfumo wa malipo mtandaoni (http//:oas.tbs.go.tz) ndani ya siku 14 kuanzia Mei 26 mwaka huu.

Shirika hilo limetahadharisha kuwa baada ya muda uliotolewa, ukaguzi utafanyika na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa mfanyabiashara yeyote ambaye atakuwa hajatekeleza maelekezo hayo.

Send this to a friend