TCAA matatani sakata la mgogoro wa uwanja wa ndege Zanzibar

0
51

Mwekezaji wa Kampuni ya Transworld Aviation FZE, Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu amefungua maombi mahakamani ya kuomba ridhaa ya kuishtaki Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) baada ya kusimamishwa kutoa huduma katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume, Zanzibar.

Hatua hiyo imekuja baada ya barua iliyotolewa Septemba 14, 2022 na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA) kuisimamisha kutoa huduma kampuni yake dada ya Transworld Aviation Limited, katika uwanja huo kituo cha tatu (Terminal Three), kuanzia Desemba Mosi 2022 na kuelekeza huduma hizo kutolewa na kampuni ya Dnata Zanzibar Aviation Services Company Limited.

LATRA: Tutawafungia madereva wa Uber na Bolt wanaofanya udanganyifu wa nauli

Hata hivyo, kutokana na mgogoro huo wa kimkataba, kampuni hiyo ya Transworld imefungua shauri la maombi katika Mahakama Kuu Masijala Kuu dhidi ya TCAA na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Aidha, katika shauri hilo kampuni hiyo imeomba ridhaa ya mahakama hiyo ili iweze kufungua shauri la maombi ya mapitio ya kimahakama dhidi ya uamuzi wa TCAA kutambua makubalino baina ya ZAA na kampuni ya Dnata ambayo pekee yake ndio imeruhusiwa kutoa huduma hiyo.

Send this to a friend