TCRA: Kampuni za simu zitakiwa kupunguza gharama za intaneti

0
45

Kutokana mlipuko wa janga la virusi vya corona kuongezeko matumizi ya huduma za intaneti, Baraza la Ushauri wa Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Tanzania (TCRA -CCC) limeziandikia barua kampuni za mawasiliano ya simu kuzitaka kupunguza gharama za intaneti.

Akizungumza na gazeti la Habari Leo, Katibu Mtendaji wa TCRA-CCC, Mary Msuya amesema baraza hilo lina jukumu la kupigania haki za watumiaji wa huduma za mawasiliano.

Amesema matumizi ya intaneti yameongezeka kutokana na watu kufanya kazi wakiwa majumbani lakini pia wanafunzi kujifunza kupitia mitandao mbalimbali.

“Kwa kuwa TCRA-CCC ina lenga kuwasaidia watumiaji wa huduma za mawasiliano kufurahia huduma hii basi ni lazima kila wanapopatwa na changamoto sisi inakuwa ni jukumu letu kuwasikiliza na kuwasaidia, hii ya kutaka kupunguzwa kwa gharama za intaneti ni kati ya mengi makubwa ambayo tumeshatekeleza,”amesema.

Ameongeza kuwa TCRA-CCC ina imani kuwa agizo hilo litafanyiwa kazi, kwa kuwa hata uamuzi wa kampuni hizo kuongeza kiwango cha utunzaji wa fedha katika akaunti za simu kutoka TZS 5 milioni hadi TZS 10 milioni, umetokana na ushauri kutoka baraza hilo.

Send this to a friend