TCRA na TRA zatakiwa kukusanya mapato ya wasanii kupitia mtandao

0
40

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,, Innocent Bashungwa ameitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kutumia teknolojia katika ukusanyaji mapato kwa njia ya mtandao kwenye kazi mbalimbali za Sanaa ili wasanii wa filamu na muziki waweze kupata haki wanayostahili kwenye kazi zao.

Bashungwa ameitaka TCRA kukusanya mapato kwa njia ya mtandao katika kazi za wasanii zinazochezwa au kuoneshwa kwenye vyombo vya Habari.

“Kuna mambo mengi ambayo TCRA mnatakiwa kusaidiana na TRA hasa kwenye ukusanyaji wa mapato wa kazi za wasanii kwa njia ya mtandao (Digital Taxation) ambayo itasaidia kupatikana kwa pesa ya kuwapa wasanii ili waweze kunufaika na kazi zao hasa kwenye mziki au filamu zinazochezwa kwenye vyombo vya mbalimbali vya Runinga na Redio,” ameeleza Bashungwa.

“TCRA, TRA na Wizara tunaweza kuisadia Serikali kwenye ukusanyaji wa mapato hasa kwa njia ya mtandao (Digital Taxation) kupitia kazi za Sanaa. Lakini pia tutawawezesha wasanii wetu kuwa na kipato kizuri ambacho watawekeza kwenye kazi zao ili kupata kazi nzuri zaidi na kukuza Sanaa nchini”, amesisitiza Mhe. Bashungwa.

Waziri aliongeza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Habari itaendelea kuifanyia maboresho COSOTA kwenye baadhi ya maeneo ili iweze kuendana na dhamira iliyopo kwenye kukuza Sanaa na kuwasaidia wasanii kupata stahiki zao zinazotokana na kazi

Send this to a friend