TCRA: Ukikutwa unatumia VPN faini milioni 5, kifungo mwaka mmoja

0
66

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka wananchi kwa ujumla na kampuni ambazo kwa asili ya majukumu na kazi zao, matumizi ya mtandao binafsi (VPN) hayazuiliki, kutoa taarifa TCRA juu ya VPN wanazotumia na taarifa zote muhimu ikiwemo anuani ya itifaki ya mtandao kabla ya Oktoba 30, mwaka huu.

Katika taarifa iliyotolewa na TCRA kwa umma, imeeleza kuwa imebaini upatikanaji wa maudhui yaliyokatazwa kwa kupitia matumizi ya mtandao binafsi (VPN) kinyume cha kanuni.

“Kanuni ya 16(2) ya Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kuhusu Maudhui Mtandaoni za mwaka 2020, mtu hatatoa, hatamiliki au hatasambaza teknolojia, programu, programu tumizi au kitu chochote kinachoendana na ambacho kinaruhusu au kumsaidia mtumiaji kupata maudhui yaliyokatazwa,” imeeleza taarifa.

Wakili feki aliyeshinda kesi zote akamatwa

Aidha, TCRA imesema itaendelea kuchukua hatua za kiudhibiti dhidi ya matumizi ya VPN yasiyo halali ikiwemo kuzuia upatikanaji wa VPN ambazo hazijatolewa taarifa au kusajiliwa na kuongeza kuwa, yeyote atakayebainika adhabu yake ni faini isiyopungua TZS milioni 5 au kifungo cha mwaka mmoja au vyote kwa pamoja.

Send this to a friend