TCRA yaifungia Wasafi FM kwa siku saba

0
40

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekifungia kwa siku saba kituo cha utangazaji, Wasafi FM kuanzia leo Septemba 11, 2020 kwa kukiuka kanuni za utangazaji.

Akitoa uamuzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amesema kituo hicho kimekiuka kanuni namba 11 ya Kanuni za Mawasiliano ya kielektroniki na Posta ya mwaka 2018 katika vipindi vya The Switch na Mashamsham.

Kilaba amekitaka kituo hicho kuomba radhi, huku akitumia nafasi hiyo kutoa rai kwa vyombo vya habari kuzingatia kanuni za utangazaji wa maudhui yenye lugha ya staha kwa Watanzania.

Send this to a friend