TCRA yaifungia Wasafi TV kwa miezi sita

0
66

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekifungia kituo cha televisheni, Wasafi TV, kutokurusha matangazo kwa muda wa miezi sita kuanzia leo Januari 5, 2021 kutokana na kukiuka Kanuni za Mawasiliano ya Kieletoniki na Posta za mwaka 2018.

TCRA imesema kuwa kanuni hizo zinataka kuzingatiwa kwa maudhui yanayorushwa na vyombo vya habari kuhakikisha kuwa yanafuata sheria.

Mamlaka hiyo imeeleza kuwa kituo hicho kilikiuka kanuni za utangazaji Januari Mosi 2021 kupitia kipindi chake cha Tumewasha Live Concert (saa 2:00 hadi 5:00 usiku) ambapo walirusha maudhui yaliyomuonesha mwanamuziki Gigy Money akitumbuiza jukwaani huku akionesha utupu wa mwili wake.

Send this to a friend