TCRA yakifungia kipindi cha Mchungaji Mwingira Star TV

0
47

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekifungia kwa miezi mitatu kipindi cha Efatha Ministry kinachorushwa kupitia kituo cha televisheni cha Star TV, kwa kukiuka kanuni za maudhui ya Utangazaji za mwaka 2018.

Uamuzi huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Habbi Gunze baada ya kusililiza ushahidi wa Efatha Ministry na Star TV.

Katika taarifa yake, kamati imeeleza kuwa kipindi hicho kinachorushwa mbashara na Mchungaji Josephat Mwingira kilitumia lugha ya dhihaka na matusi dhidi ya mamlaka ya juu ya nchi.

Mbali na adhabu hiyo, TCRA imetoa onyo kali kwa kituo hicho na kukitaka kuwaomba radhi watazamaji wake na umma kwa ujumla kwa siku tatu kuanzia Januari 25 hadi 27 mwaka huu.

Kutokana na  kurushwa kwa kipindi hicho, TCRA  imeeleza Star TV wameonesha udhaifu katika kusimamia vipindi mbashara hivyo kuruhuu maudhui yenye ukakasi kutifikia jamii kinyume na kanuni ya 37 (1) (a) ya kanuni za mawasiliano ya kielekroniki na posta ya Utangazaji wa redio na Televisheni ya Mwaka 2018.

Send this to a friend