TCRA yaufungia wimbo wa Diamond na Zuchu

1
65

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) limewataka vyombo vya utangazaji kutopiga video ya wimbo wa msanii Nasib Abdul (Diamond Platnum) alioshirikiana na Zuhura Othuman (Zuchu) kutokana na video kwenda kinyume na maadili ya kidini.

Inadaiwa wimbo huo unaofahamika kama ‘Mtasubiri sana’ umeleta ukakasi miongoni mwa waumini wa dini au madhehebu fulani baada ya kuonyesha wahusika wakiimba kwaya kanisani kisha kuacha na kuelekea kwingine baada ya kupigiwa simu.

Aidha, TCRA imeagiza vyombo vya utangazaji na mitandao ya kijamii hapa nchini kutorusha video ya wimbo huo hadi msanii huyo atakaporekebisha sehemu hiyo ya video.

Ujumbe mkubwa katika wimbo huo ni kuwaambia wale wote wanaosubiri wawili hao waachane kuwa watasubiri sana, kwani hawatoachana.

Send this to a friend