TCRA yavionya vyombo vya habari kuhusu taarifa za kidini za kufikirika

0
10

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekemea vikali taarifa za kufikirika na zenye utata kuhusu imani za kidini ambazo zinaendelea kushamiri kwenye vyombo vya utangazaji mitandaoni, na vile vya runinga na redio za kawaida (traditional media), na kuviagiza vyombo hivyo kuacha mara moja.

TCRA imetoa ufafanuzi kuwa taarifa zinazohusu mawazo ya kufikirika yanayolenga imani za kidini ni masuala binafsi ya mtu, hivyo mahali sahihi ya kutoa mawazo hayo ni kwenye nyumba za ibada na sio kwenye vyombo vya habari na utangazaji, kwani vyombo hivyo vina wajibu wa kufuata misingi na maadili ya taaluma zao kwa kutoa taarifa zilizofanyiwa uchambuzi, za kuaminika na za kweli.

“Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Maudhui ya Utangazaji wa Redio na Televisheni), 2018 na Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Maudhui ya Utangazaji Mtandaoni), 2022 zimeelekeza watoa huduma ya utangazaji kujiepusha na maudhui ya upotoshaji yanayogusa imani za watu.

Taarifa ya Serikali kuhusu ugonjwa wa Marburg uliozuka Kagera na namna ya kujikinga

Hivyo basi, taarifa zozote zinazotolewa kwa umma kupitia vyombo vya utangazaji ziwe za ukweli, uhakika na zitoke katika vyanzo vinavyoaminika ili kuepusha upotoshaji kwa jamii,” imeeleza taarifa.

Aidha, TCRA imesema itachukua hatua kali za kisheria kwa chombo chochote cha utangazaji ambacho kitabainika kuendelea kurusha taarifa zenye maudhui kama hayo.

Send this to a friend