TECNO kuwapa furaha Watanzania msimu wa Sikukuu na Kombe La Dunia

0
39

‘’Tunajua Kombe la Dunia ni la kusisimua lakini msimu wa Krismasi na likizo unakuja, je, unafikiria nini unaweza kumpa mpendwa wako? TECNO inakukumbusha kuwa watu hawa wana maana kubwa kwako kuliko kitu kingine chochote, andaa zawadi za kushiriki nao furaha, Shinda TECNO CAMON 19 mpya katika kila mechi kwa uwapendao msimu huu wa sikukuu’’,

 

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi balozi wa kampeni hii Mbwana Ally Shomari mchezaji wa Taifa Stars anayekipiga katika Club ya Yanga.

Meneja Masoko TECNO, Salma Shafii amesema kuwa, ‘’sambaza furaha kwa kupost picha ya umpendae ukiambatanisha na ujumbe mzuri wa upendo kisha #Sambazafuraha jaribu kadri uwezavyo na kama ambavyo kila mechi inamshindi basi ndivyo hivyo hivyo juhudi yako itakupa ushindi wa kumzawadia umpendae TECNO Camon 19 na mshindi kutangazwa live @tecnomobiletanzania Kila siku’’.

 

Mariam Mohamed, Meneja Mauzo TECNO kanda ya Dar es Salaam ameeleza kuwa pamoja na kampeni ya sambaza furaha lakini pia siku hii ya leo tunazindua na promosheni ya Zigo la Disemba na kutaja zawadi ambazo zitaenda kwa wateja katika kipindi hiki nazo ni pikipiki, TECNO Camon 19, Spark 9, Headset, mabag na Miamvuli.

“Promosheni ya kwanza inafahamika kwa jina la “Zigo la Disemba” ambayo itahusisha utoaji wa zawadi za papo kwa hapo nazo ni headset,mabag na miamvuli, zawadi kila week nazo ni Camon 19 au Spark 9 na Zawadi ya Mwezi nazo ni pikipiki kwa wateja wa TECNO Camon 19 na Spark 9 wataofanya manunuzi ya simu hizo ndani ya msimu huu wa sikukuu’’.

 

TECNO Camon 19 na Spark 9 ni simu bora ambavyo zimekuwa zikifanya vizuri tangu kuingia kwake nchini Tanzania. TECNO Camon 19 imejizolea tuzo ya if DESIGN AWARDS kutoka na muonekano wenye kuvutia machoni, Camera ya MP64 inaifanya kuwa chaguo bora kwa photographers na vijana wenye kujihusisha na biashara za mitandaoni sifa nyengine za simu hii ni battery 5000Mah na processor yenye kuchakata kazi kwa haraka MediaTek G96.

TECNO Spark 9 ni simu ya vijana wote wakishua inakitunza kumbukumbu cha GB 128 na kioo kipana cha inch 6.6 na refresh rate 90 ambavyo huumpa uhuru wa kuhifadhi na kujisomea vitabu kwa nafasi pamoja na pia inadumu na chaji kwa muda mrefu ikiwa na mAh5000.

 

Uzinduzi wa promosheni hizi ni muendelezo wa mikakati ya kampuni ya TECNO Tanzania kuwapa furaha wateja wake katika kipindi cha mwisho wa mwaka kwani imekuwa ikifanya hivyo mara kwa mara inapofika kipindi hiki.

Kwa huduma ya haraka wasiliana na 0744545254, 0678035208 au tembelea @tecnomobiletz twitter, @tecnomobile facebook au @tecnomobiletanzania IG.

 

 

 

 

 

 

Send this to a friend