Tecno yakabidhi zawadi ya TZS milioni 5 kwa mshindi wa promosheni ya Spark 8C

0
38

Kampuni ya simu ya TECNO imehitimisha rasmi promosheni ya simu ya SPARK 8C baada ya kukabidhi zawadi ya milioni 5 pesa taslimu za kitanzania kwa mshindi anayefahamika kwa jina la Mohammed Khatibu.

Meneja mauzo TECNO akiwa anaelezea kuhusu promosheni ya SPARK 8C

Meneja Mauzo wa TECNO, Bi. Mwamvua Hussein Kapesula alizungumza na kusema, “Niko mbele yenu leo kukabidhi zawadi ya shilingi milioni 5 kwa mshindi wa promosheni ya SPARK 8C ambaye ni ndugu Mohammed Khatibu.

Meneja Mauzo wa TECNO akiwa anakabidhi zawadi kwa mshindi

Promosheni hiyo ilizinduliwa rasmi mnamo mwezi April na kudumu kwa muda wa mwezi mmoja na mshindi alitangazwa live kupitia @tecnomobiletanzania mnamo tarehe 24/05/2022.

Ndugu Mohammed Khatibu ambaye ndiye mshindi wa promosheni hiyo alionyesha furaha yake kwa kusema “Kwa kweli nilijiskia furaha kubwa baada ya TECNO kunipigia simu na kunieleza nimeshinda millioni 5 baada ya kununua simu ya SPARK 8C na hatimaye leo kukabidhiwa zawadi hiyo. Nilikuwa na ndoto ya kufungua maabara yangu na napenda kuwashukuru TECNO kwa kuwa sehemu ya kufanikisha ndoto yangu hiyo.”

Ndugu Mohammed Khatibu akiwa amekabidhiwa zawadi

Kadhalika, afisa mahusiano wa TECNO, Bi. Prisca Ernest alitoa shukrani zake kwa kusema, “Shukrani nyingi ziwafikie wateja wetu wote wa TECNO walioweza kufika katika maduka yetu yote nchini Tanzania na kununua simu hii ya SPARK 8C na hata simu zetu nyingine pia”.

Wafanyakazi wa TECNO wakiwa na hundi ya mshindi

Send this to a friend