Teknolojia inavyoleta mapinduzi katika sekta ya bima ya afya

0
37

Mwezi uliopita Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akihutubia Bunge aliwasihi Watanzania kujiunga na mifumo ya bima za afya.

Katika maelezo yake Waziri alisisitiza kuwa, endapo wananchi watajiunga na mifumo hii na kupata bima za afya, wataweza kupata matibabu wakati wowote pasi na kuhofia uwepo wa fedha.

Inafahamika kuwa upatikanaji wa huduma za afya za msingi kwa kila Mtanzania ni lengo moja la Mpango wa Maendeleo wa Taifa kufikia mwaka 2025.

Serikali imekuwa ikifanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa watu katika pande zote za nchi wanapata huduma za afya zenye unafuu.
Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la watoa huduma za afya binafsi nchini Tanzania. Kampuni kutoka sekta binafsi wametumia fursa ya teknolojia ya kidijitali kuboresha upatikanaji wa huduma za afya na kuepuka changamoto mbalimbali.
Uwekezaji kwenye huduma za afya kupitia simu za mkononi umekuwa na matokeo chanya kwa watu, na hivyo kuimarisha nguvu kazi ambayo imekuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi.

Tigo Tanzania ni moja ya kampuni ambazo zimekuwa mstari wa mbele katika utoaji wa huduma za afya kwa mifumo ya kielektroniki.
Huduma ya Tigo Bima inawasaidia watu kutoka maeneo mbalimbali nchini kuweza kupata huduma za afya zilizo bora bila kuathiri mipango yao mingine ya kifedha.

Mtu yeyote anayetumia laini ya Tigo anaweza kujiunga na huduma mbalimbali kama vile, Maisha, ajali, na bima ya kulazwa hospitali, kwa ajili ya kujigharamia wao wenyewe pamoja na familia zao.

Pia, endapo mteja wa Tigo atalazwa hospitali, watapatiwa fedha kwa siku zote ambazo atakuwa amelazwa. Huduma kama hii inawasaidia wateja wa Tigo kuwa na mpango wa muda mrefu wa huduma za afya kuliko kushtukizwa au huduma za gharama kubwa.

Kampuni kama Tigo inaonesha kuwa teknolojia ina nafasi kubwa sana katika kuimarisha huduma za afya. Huduma kama hizi kwa kushirikiana na serikali zinaweza kuwasaidia wananchi wengi kupata huduma bora na kuimarisha mifumo ya afya.

Nafasi kama hizi zinaweza kusaidia kusukuma mbele maendeleo ya Tanzania na kuhakikisha inafanikisha lengo lake la mwaka 2025.

Send this to a friend