Teknolojia inavyotuwezesha kuendesha maisha na biashara
Hali inaonesha kwamba, nchi nyingi duniani zimeathirika na homa ya kirusi cha korona na athari hizi huenda zikabaki katika maisha ya watu kwa muda mrefu.
Mbali na njia mbalimbali za kupambana na maambukizi kama kufunga shule na kuzuia mikusanyiko, Watanzania wengi pia sasa wanatumia njia za kidijitali zaidi kuwasiliana na kuendesha maisha na shughuli zao za kila siku kwa sababu maisha lazima yaendelee. Ama kweli sasa kuungana kidijitali limekuwa jambo muhimu sana.
Mawasiliano ya kidijitali yameleta ahueni sana. Mfano wapo watu ambao hawataweza kuwatembelea ndugu, jamaa na marafiki kama walivyozoea lakini sasa wanaweza kuwasiliana kwa simu na kubaki wamoja na wapendwa wao. Jambo hili linaelezwa kuwa ni muhimu kwa afya ya akili.
Teknolojia ya kidijitali imekuwa si tu ya faida kwa mawasialiano ya mtu mmoja mmoja na familia bali pia kwa biashara. Imesaidia biashara hizi kuendelea kutoa huduma kupitia mtandao wa intaneti ikiwemo kuwasiliana na wateja, huduma za masoko na malipo kidijitali.
Kwa bahati nzuri kampuni za mawasiliano ya simu ziko mstari wa mbele kuwezesha sisi kubaki tumeungana kidijitali. Kampuni ya Tigo kwa mfano ina huduma ya router ya intaneti nyumbani (Home Internet Router) ambayo inasaidia familia kuwasiliana kwa kuipa mtandao bora wa intaneti. Kwa upande wa maofisi nao wana huduma ya intaneti kwa ofisi (Office Internet) ambayo husaidia ofisi kuendelea kubaki pamoja na kufanya kazi kidijitali.
Katika nyakati hizi za changamoto, kubaki tumeungana kidijitali na kuendelea na maisha na shughuli zetu ni jambo muhimu kuliko wakati wowote ule.