Teknolojia ya Kidijitali ilivyo fursa ya kukuza uchumi endelevu Tanzania
John Mtambalike, DIT
Katika miaka ya hivi karibuni, teknolojia ya kidijitali nchini Tanzania imezidi kukua na kulisaidia taifa hili kuwa moja ya taifa linalokuwa kwa kasi kwenye eneo la teknolojia ya kidijitali Afrika Mashariki. Ni wazi kuwa ukuaji huu umechangia kwa kiasi kikubwa kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi, na vijana wengi wameweza kufaidika.
Katika sekta nyingine, teknolojia ya kidijitali zinatoa fursa kubwa zinazopelekea ubunifu na kupelekea ukuaji endelevu. Kwa mfano, juma hili, Wizara ya Kilimo ilichangia vifaa mbali,mbali vya TEHAMA katika taasisi mbalimbali za mafunzo ya kilimo zikiwemo binafsi na zile za serikali ili kurahisisha shughuli za mafunzo.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya mchango huo utasaidia kufanya shughuli kidijitali katika taasisi hizo pamoja na kurahisha ufundishwaji wa vizazi vijavyo vya wafanyakazi.
Licha ya teknolojia kuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya kiuchumi, ni muhimu kufahamu kuleta mabadiliko ya kiteknolojia kunahita ushirikiano kati ya wadau wa sekta binafsi na serikali.
Kwa bahati nzuri, Sekta ya mawasiliano ya simu nchini Tanzania zimejiweka katika mazingira mazuri ya kusaidia mabadiliko hayo.
Kwa miaka mingi sasa kampuni mbalimbali kama Tigo Tanzania zimewekeza katika biashara ya kidijitali nchini Tanzania katika nyanja zote za maisha ikiwa ni pamoja afya, malipo ya mtandaoni na mawasiliano.
Mwaka jana ilitangazwa kuwa Tigo inaungana na kampuni ya Zantel. Hii ni habari njema zaidi katika sekta ya kidijitali nchini Tanzania.
Muungano huo unatoa fursa kwa wateja wa Tigo na Zantel. Mara muungano huo utakapokamilika wateja watanufaika na miundombinu iliyoboreshwa.
Aidha, wateja watanufaika na wigo mkubwa wa huduma mbalimbali ambazo zitasaidia kukuza upatikanaji wa huduma za fedha kwa njia ya simu na huduma nyingine za intaneti.
Tushukuru na kufurahia kazi kubwa iliyofanywa na sekta hii kutokana na mchango wake unaonufaisha wengi.