Teknolojia ya mawasiliano ni nguzo muhimu ya ukuaji wa biashara nchini

0
33

Lengo la taifa la maendeleo linaelezea namna ambavyo biashara ndogondogo na za kati (SMEs) ni muhimu katika uchumi. Inakadiriwa kuwa SMEs zina jumla ya biashara milioni 3 ambazo kwa pamoja zinachangia zaidi ya asilimia 25 ya pato la taifa (GDP).

Kutokana na hali hiyo, ni muhimu kuhakikisha sekta hii inaendelea kukua.

Tunapojadili SMEs ni ukweli usiopingika kuwa sekta ya mawasiliano ni muhimu kwa ukuaji wake. Makampuni ya mawasiliano ya simu hutupatia huduma za vifurushi vya data, kutuwezesha kuwasiliana kibiashara, au na rafiki zetu na familia kwa urahisi, na programu tumishi (apps) za makampuni hayo hurahisisha maisha yetu.

Msingi wa biashara ni mawasiliano na taarifa kati ya mnunuzi na muuzaji na makampuni ya mawasiliano nchini Tanzania, kwa kiasi kikubwa yanasaidia jumuiya ya wafanyabiashara.

Kwa mfano, Tigo ilikuwa moja ya kampuni za kwanza kujiunga na mfumo wa malipo wa serikali (Government’s e-Payment Gateway). Kwa kushirikiana na serikali, Tigo imewarahisishia sana wafanyabiashara kulipa ankara zao.

Programu tumishi kama vile Tigo Pesa zimewasaidia pia wafanyabiashara kukusanya malipo ya bidhaa zao. Wateja sasa wanaweza kulipia bidhaa zao kwa kutumia programu ya Tigo Pesa, au hata kuwalipa wafanyakazi wao. Inakadiriwa kuwa zaidi ya kampuni 70,000 zinatumia huduma za tigo kwa minajili hii.

Pamoja na hayo, Tigo imezindua njia ya huduma kwa wateja kwa kutumia WhatsApp ambao ni pamoja na wateja wa kibiashara. Huduma hiyo inawawezesha wateja kuwasiliana na dawati la huduma kwa wateja kwa urahisi na haraka kuhusu tatizo lolote.
Kadiri idadi ya SMEs na mchango wake katika uchumi unavyozidi kuongezeka, ni jambo jema kuona makampuni ya mawasiliano yakifanya kazi kutoa huduma kwa pamoja.

Send this to a friend