TEMESA: Tumieni Daraja la Nyerere kuepuka usumbufu

0
32

Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) umewaomba radhi watumiaji wa kivuko cha MV. Magogoni kutokana na kusindwa kutoa huduma.

Katika taarifa yake iliyotolewa kwa umma, TEMESA imesema leo Juni 2, kivuko hicho kimeshindwa kutoa huduma kwa sababu za hitilafu zilizojitokeza kwenye mifumo ya uendeshaji wa kivuko hicho.

Aidha, taarifa hiyo imeongeza kuwa shughuli za uvushaji abiria zinaendelea kwa kutumia kivuko cha MV. Kigamboni na kuwashauri abiria kutumia njia mbadala ya Daraja la Nyerere ili kuepusha usumbufu.

Send this to a friend