Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) umesema changamoto kubwa zinazoikabili kwa sasa ni nauli za vivuko ambazo zimepitwa na wakati na zisizoendana na bei ya soko wala gharama halisi za uendeshaji wa vivuko.
Hayo yameelezwa na Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Lazaro Kilahala wakati akizungumza na waandishi wa habari jiini Dodoma juu ya majukumu mbalimbali ya TEMESA na utekelezaji wa bajeti ya Serikali kwa wakala huo wa mwaka 2022/23.
“Sote tunafahamu gharama za uendeshaji wa hivi vitu vimeongezeka. Mwaka uliopita peke yake wastani lita moja ya dizeli peke yake iliongezeka kama shilingi mia saba na kitu ndani ya mwaka mmoja. Hiyo ni licha ya Serikali kufanya jitihada kubwa kuweka ruzuku kwenye mafuta,” ameeleza
Nape: Tutadhibiti usambazaji picha za ngono mitandaoni
Kwa mujibu wa Kilahala, mahitaji ya mafuta ya dizeli kwa ajili ya kuendesha vivuko vyote ni lita 210,000 kila mwezi ambapo kutokana na ongezeko la bei za mafuta imepelekea ongezeko la gharama za uendeshaji takribani milioni 150.
Aidha, kiongozi huyo amesema tayari wanaendelea na mazungumzo na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ili kuangalia upya nauli za sasa.
TEMESA ina jukumu la usimamizi na uendeshaji wa vivuko vyote vya Serikali vilivyopo maeneo mbalimbali 22 ya nchi.